Wednesday , 7th May , 2014

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya na mmiliki wa studio ya MJ ambaye kwa sasa hivi anajishughulisha zaidi na mambo mengine pembeni ya kutayarisha muziki, Master J, leo hii ameshiriki katika Kikaangoni Live ya ukurasa wa facebook wa EATV.

Master J

Enewz tulipata fursa ya kuongea na Master J baada ya zoezi la Kikaango, Live na kufunguka kama hivi ambapo amesema kuwa, amepata kufahamu ni kwa namna gani watu wanavyomuelewa tofauti, na pia ameweza kujifunza mengi juu ya namna ya kukaa na mashabiki kwa njia ya maswali na pia madongo ambayo hayakukwepeka kumpata.

Master J ambaye hapo zamani alikuwa akifahamika kama Rap Master J amesema kuwa, kupitias Kikaango ameshangazwa na namna watu wanavyomhusisha na mahusiano ya kimapenzi na Madam Ritha, Salama na wengineo, ambapo pia ameahidi kutoa maelezo rasmi juu ya mahusiano yake na Sarah Kaisi ama Shaa siku za Karibuni.

Master J akakiri kuwa, angefahamu namna Kikaango kilivyo na changamoto ya maswali na mitizamo tofauti ya watu, angejipanga zaidi kabla ya kuja kukabiliana nacho.

Mster J anamaliza hivyo, na sasa macho yote yanaitazama wiki ijayo kwa hamu kubwa kufahamu atakuwepo staa gani kwa ajili ya kuchat nae LIVE, endelea kuifuatilia, like na share na marafiki ukurasa huu wa www.facebook.com/eatv.tv kwa burudani kama hii na nyingine kali.