Thursday , 16th Jun , 2016

Msanii Hakeem 5 amewafungukia mapendehsee wenye tabia ya kujipenyeza kwa wasanii wanapokuwa kwenye chati, na kuwakimbia wakiwa wameshuka kimuziki.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Hakeem 5 amesema watu hao sio wazuri kwao kama wasanii, hivyo wanafanya juu chini kuwaepuka, kwani hawapendi mafanikio yao.

“Mapedeshee wanaangaliaga upepo, unajua kuna watu wengine wanakuwa hawajui thamani yako, mtu mwengine akishaona ushapotea wewe unamtafuta unataka labda akusapoti, anaweza kuona huyu ameshaisha huyu, anaangalia watu ambao wanafanya vizuri, mwisho wa siku ukirudi ye akawa anakutafuta unaona huyu jamaa ni snitch, sio mtu ambaye anataka kuona mi nafika pale, kwa hiyo watu kama hawa si tunawaepuka kwa sababu sio watu wazuri wanakupenda kwa sababu ya kitu”, alisema Hakeem 5.

Pia Hakeem 5 ameeleza sababu ya yeye kukaa kimya sana huku wenzake alioanza nao game kuendelea kutoboa akiwemo Alikiba, na kusema kwenye game lazima wapishane, lakini ana imani atarudi tena.

“Kiukweli wote sisi ni wamoja na kazi kila kitu kinaenda kwa time lazima tupeane muda, mi nilipotea lakini nitarudi vile vile”, alisema Hakeem 5.