Karibu Music festival
Zoezi la maombi ya kushiriki katika tamasha hilo linafanyika kwa njia ya mtandao likihusisha wasanii wale wanaofanya muziki wa Live.
Karibu Music Festival ambayo pia hutoa nafasi ya mafunzo kwa watakaoshiriki, kwa mwaka 2015 itafanyika kwa siku tatu mfululizo kuwanzia tarehe 6 mpaka 8 mwezi Novemba 2015 na kuhusisha wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania.