Wednesday , 22nd Apr , 2015

Katika kuendelea kuuboresha muziki na kuuongezea ladha na viwango vya juu, mtayarishaji muziki Man Water ameweka wazi kuwa anajipanga kuingia katika kurekodi muziki wa live kupitia studio yake.

mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Man Water

Hii ni moja ya hatua yake mpya kwa mwaka huu ambayo pia itaongeza wigo wa aina ya wasanii atakaokuwa akifanya nao kazi.

Man Water amesema kuwa, mpango huo upo katika mchakato na pindi utakapokamilika atatoa taarifa rasmi kwa wadau na wapenzi wa muziki ambao anatayarisha, akiwa kama mtayarishaji mwenye rekodi ya kushinda tuzo kadhaa hapa Bongo.