Thursday , 20th Apr , 2017

Msanii wa 'Singeli' Khalid Starboy ambaye sasa yupo chini ya usimamizi wa G Maker amefunguka na kusema 'hit maker' wa ngoma ya Hainaga Ushemeji Man Fongo ni kama amemkimbia baada ya yeye kujiunga chini ya usimamizi wa G Maker.

Man Fongo (kushoto) na Starboy

Khalid Starboy aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na EATV na kusema alitegemea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Man Fongo na kusema umoja wao huo ungeleta maana zaidi lakini sasa Man Fongo alipoona ameingia huko yeye akakimbia.

Khalid amekuwa msanii wa tatu kupita katika mikono ya G Maker ambaye alianza kumsimamia kazi Sholo Mwamba, Man Fongo na sasa anamsimamia msanii huyo Khalid Starboy 

Mtazame hapa Khalid akifunguka mengi zaidi: