Friday , 27th Nov , 2015

Maziko ya mama wa nyota wa muziki Size 8 kutoka nchini Kenya, yamepangwa kufanyika huko Mbale Uganda baada ya misa na tukio la kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kufanyika jana huko Kenya.

Size 8

Mpango wa kukamilisha msiba na maziko ya mama huyo huko Uganda ni kutokana na asili ya baba wa msanii huyo, Samuel Munyali ambaye ana uraia wa Kenya na vilevile Uganda ambapo ndipo asili yake.

Kifo cha mama wa Size 8 ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la figo kilitokea ijumaa iliyopita ikiwa ni takriban siku tatu baada ya msanii huyo kujifungua mwanae wa kwanza wa kike ambaye amepatiwa jina la Belle.

Tags: