Thursday , 17th Sep , 2015

Kundi la muziki la Makomando, limekuwa moja ya makundi ya wasanii ambalo limepata shavu la kuwa mabalozi wa kupambana na gonjwa la malaria, ambapo kwa sasa wapo huko mikoa ya kusini kwa ajili ya kufanyakazi hiyo.

Kundi la muziki la Makomando, Muki pamoja na Freddywine

Makomando wamewataka watanzania kutokujisahau kuwa, gonjwa hilo bado ni hatari, lipo na linapukutisha maisha, mapokezi mazuri wanayoendelea kuyapata huko kusini kwa sasa yakiwa ni ishara tosha kuwa somo kwa wananchi kuhusiana na gonjwa hilo linaendelea kueleweka vizuri.

Kuhusiana na hilo, Muki pamoja na Freddywine kutoka Makomando hapa wanaeleza;