Tuesday , 1st Jul , 2014

Mwanamuziki maarufu wa nchini Tanzania Vitali Maembe ameiambia eNewz kuwa hivi sasa ameelekeza nguvu zake kuwafundisha muziki watoto pamoja na vijana katika vituo vilivyopo Bagamoyo, Pangani na Dar es Salaam.

Mwanamuziki Vitali Maembe

Maembe ambaye ni mahiri wa kutumia gitaa amesema kuwa pamoja na kuwafundisha vijana hao nchini, pia anatoa mafunzo ya muziki aina ya Dance na African Traditional Music kwa watoto wa nchi za Norway, Sweden na Ujerumani.

Maembe ambaye anavuma Afrika na bendi yake inayoitwa The Spirits, pia kwa sasa yupo katika maandalizi ya kutoa albamu yake ya nne mwezi Agosti mwaka huu.

Maembe ambaye ni moja ya wanamuziki maarufu wa mashairi anayefanya muziki wa asili na pia miondoko ya Pwani kwa sasa anafanya vyema na albam zake tatu zikiwemo Bagamoyo aliyoitoa mwaka 2004, Imbila 2007 na Chanjo 2010.