Monday , 23rd Feb , 2015

Aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo fleva, marehemu Moses Bushagama a.k.a Mez B amezikwa leo katika makaburi ya Muhanga Maili Mbili huko Mkoani Dodoma, katika safari yake ya mwisho iliyohudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji.

Jeneza la Msanii Mez B

Shughuli za kuuaga mwili wa msanii Mez B zimefanyika Viwanja vya Mashujaa huko Dodoma ili kutoa nafasi kwa watu wengi zaidi kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu ambaye enzi za uhai wake alikwishawahi kuzitikisa chati za muziki kwa rekodi kadhaa kali kama vile ya 'Kama Vipi', Kikuku na nyinginezo.

Hili linakuwa ni pigo jingine kubwa kwa sanaa ya muziki Tanzania na vilevile kwa kundi la Chamber Squad ambalo linapoteza msanii wa pili sasa, na eNewz tunamuomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Aamin.