Saturday , 29th Mar , 2014

Msanii wa muziki kutoka Marekani, Madonna anatarajia kuhusika katika kazi ya kuongoza filamu ambayo itafanyika huko Kenya, ikiwa inakwenda kwa jina Ade: A love Story ambayo kisa chake kinatokana na kitabu cha hadithi cha mwandishi Rebecca Walker.

Madonna

Filamu hii ya Mapenzi ni juu ya binti wa kimarekani wa miaka 19 ambaye alifika katika pwani ya Kenya na kuangukia katika penzi la kijana anayeitwa Ade, na kuanzisha mahusiano ambayo yanakumbana na vikwazo mbalimbali.

Filamu hii inaongeza rekodi ya filamu ambazo Madonna amekwishashiriki kuongoza, ikiwepo ile ya W.E. na Wallis Simpson and Filth and Wisdom.