Monday , 14th Nov , 2016

Msanii wa bongo fleva Madee amesema muda wake wa kuoa bado na hawezi kuoa kwa sababu wenzake wameoa au kwa sababu Tunda kamuahidi kumtolea mahari bali ataoa atakapokuwa tayari kufanya hivyo.

Madee

 

Akiongea ndani ya eNewz Madee amesema Tunda hawezi kumpangia wakati wa yeye kuoa kwa kuwa yeye ameoa "mimi naheshimu sana neno ndoa na ntaoa ntakapoona kwamba nipo tayari ki akili kimawazo na hata vitedo" aliendelea kusema  ataoa atakapokuwa kamaliza mambo yote ili atakayemuoa ajulikane kuwa ndiyo mke wake na hatakubali ndoa yake kuwa na kashfa yeyote

Hata hivyo Madee alimsihi Tunda kuweka pesa ambayo ameahidi kumlipia katika mahari yake ili ikifika muda wa kuoa basi Tunda aweze kumtolea hiyo mahari kwa kuwa dini ya kiislam inaruhusu ndugu wa kiislamu kutoleana mahari.