Monday , 23rd Mar , 2015

Msanii wa muziki Madee, amezungumzia mabadiliko makubwa ambayo yanaonekana sasa katika muziki wake kuangalia zaidi soko, huku akitoa angalizo kwa wasanii kuangalia sana namna wanavyobadilika kutokana na hatua hiyo.

Staa huyo amesema kuwa, kwa upande wake ameweza kutengeneza alama kwa upande wa midundo ya Kwaito, akieleza kuwa ni muhimu kwa wasanii kubadilisha biashara zao kwa kupima ni nini mashabiki wanapenda ili kuweza kufanikiwa katika muziki.