Wednesday , 15th Apr , 2015

Staa wa muziki Mabeste, ameweka wazi tatizo kubwa la kiafya la mkewe Lisa, ambaye kwa muda unaofikia miaka miwili na nusu sasa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kubanwa na pumzi na kuishiwa nguvu, moyo kwenda mbio hata kupelekea kupoteza fahamu.

msanii wa bongofleva Mabeste na mkewe Lisa

Staa huyo wa muziki amewataka mashabiki na watu wake wa karibu kushiriki naye katika kipindi hiki kigumu ambapo yeye binafsi amesitisha kazi zake zote zinazomuingizia kipato kumuuguza mkewe, ili kufanikisha kupata vipimo vikubwa zaidi na matibabu kuweza kurejesha hali yake ya kawaida.

Pole sana kwa Mabeste kwa kuuguliwa na mkeo.