Wednesday , 10th Dec , 2014

Mkali wa michano kutoka kundi la Mabaga Fresh, JB amesema kuwa kwa sasa katika muziki ushawishi wao katika 'Industry' ya Bongofleva, umeyumba na pengine kupungua zaidi kutokana na mipango yao mingi kukwamishwa.

msanii wa bongo fleva JB kutoka kundi la Mabaga Fresh

Akiongea kwa hisia, JB amesema sababu kubwa wanayoiona wao ikiwa ni hali yao ya ulemavu akiweka wazi kwamba kazi zao wanazifanya vizuri kama kawaida, isipokuwa sapoti imekuwa ndogo kiasi cha wao kukosa hata msimamizi wa kazi zao, kitu kinachowazuia kurudi katika chati kama kipindi cha nyuma ambapo walikuwa gumzo kubwa.