Lord Eyes
Lord Eyes amesema kuwa changamoto kama za madawa ya kulevya, kupelekwa polisi kwa matendo ya kihalifu ni mambo ambayo mama yake mzazi alihisi yameletwa na muziki kitu ambacho kilikuwa kikimnyima furaha zaidi mama yake.
"Mama yangu mimi ni mtu anayeniamini sana. na ananijua nilikuwa genious toka nasoma mpaka nimemaliza sijawahi kumpelekea matokeo mabovu. Sasa baada ya matatizo kutokea mama yangu ndiye alikuwa anaumia zaidi kwa sababu alikuwa anajua hata bila muziki ningefanya kazi yoyote nzuri. alikuwa anashindwa kuniambia direct acha muziki kwa sababu yeye mwenyewe anapenda muziki na ni muimba kwaya. Kwa ujumla familia nzima kwetu inapenda muziki ndiyo maana walikuwa wananisapoti." Alisema Lord Eyes.
Aidha Lord Eyes amewatoa wasiwasi mashabiki zake kuhusu kuendana na upepo wa soko la muziki kwani yeye binafsi anaamini muziki ni fashion hivyo ana uwezo wa kwenda nalo sawa.





