Monday , 6th Jun , 2016

Msanii wa kike nchini Linah Sanga amefunguka juu ya kile kinachoonekana kwenye Page zake kumsapoti mara kwa mara Msanii mwenzake Billnass ambae kuna uvumi mkubwa kuwa wanatoka kimapenzi kwa siri.

Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga

Akizungumza na Enewz Linah alisema kuwa Billnas ni msanii mwenzie na kwa kuwa ameshashuti video ya ngoma yake alimuomba aweke linki ya video yake katika bio yake hivyo hakuwa na budi kufanya havyo na wala hakuna kitu kingine chochote.

“Ni swala tu la kimuziki kwasababu aliniomba harafu siko peke angu kuna wasanii wengine nao wamemuweka na kuna watu maarufu pia ambao sio wasanii wamemuweka kama petiti man”,alisema Linah.