Tuesday , 5th Jan , 2016

Msanii Koba MC aliyeibukia katika muziki kutoka kundi la 'Watu Pori' wakiwakilisha Morogoro, ameeleza kuwa ukaribu wake na vilevile uwezekano wa yeye kufanya kazi na Afande Sele ambaye amemuweka katika ramani ya muziki haupo tena.

Msanii Koba MC kutoka kundi la 'Watu Pori' kutoka Morogoro,

Mkali huyo ameyaeleza haya kutokana na mabadiliko ya gemu na hatua ya Afande kuuweka pembeni muziki kitu ambacho kimepunguza mukari wa kufanya kazi pamoja na nguli huyo.

Koba ameieleza eNewz kuwa, mitindo ya muziki inayofanyika sasa, na mabadiliko makubwa yenye lengo la kumtafutia mashabiki tofauti zimemuweka tofauti na Afande Sele, binafsi akiwa sasa anakomaa kutengeneza kazi zake kuendana na kasi na mabadiliko ya kisasa katika gemu.