Tuesday , 6th Oct , 2015

Star wa muziki Maurice Kirya wa Uganda amegawa faida anayopata kutoka katika biashara ya mgawaha anayofanya, ambapo atakuwa akichangia kiasi cha pesa kutoka mauzo yake kusaidia harakati za kuongeza uelewa wa tatizo la ugonjwa saratani nchini humo.

Staa wa muziki Maurice Kirya wa Uganda

Maurice anaingia katika harakati hizo akiwa pia ameguswa kwa namna ya kipekee baada ya kumpoteza mama yake mzazi hivi karibuni kwa ugonjwa huo, akiunganisha harakati zake na shirika lisilo la kiserikali la Uganda Women’s Cancer Support Organization kufikisha elimu kwa watu na kupeana moyo.

Maurice atakuwa akitekeleza zoezi hilo kwa mwezi huu mzima wa Oktoba ambao unatambulika kama mwezi wa kuongeza uelewa juu ya saratani ya matiti kwa mwaka huu.