Thursday , 19th Nov , 2015

Nyota wa muziki King Saha wa nchini Uganda amepata wakati mgumu wa maisha yake baada ya kuzushiwa kifo, taarifa zilizosambaa kwa kasi kubwa kwa njia ya mitandao na kumuacha na kazi kubwa ya kuwaaminisha watu kuwa yupo sawa sawa.

Nyota wa muziki King Saha wa nchini Uganda

Taarifa hizo za kushtusha zilianza kupitia post ambayo iliwekwa katika mtandao wa facebook na watu wasiojulikana, ikinukuliwa na kusambaa na baada ya kumfikia King Saha mwenyewe, alilazimika kutoa maelezo ya kuwahakikishia ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki kuwa yupo hai na anaendelea na ratiba zake.

Kama ilivyo kwa Mastaa wengine katika hali kama hii, hisia pia zimesambaa kuwa huenda King Saha mwenyewe akawa ndio chanzo cha taarifa hizo akivuta akili za watu kuwatayarisha na ujio mpya baada ya kufanya vizuri na rekodi kama Bbera Awo na Science kati ya nyingine nyingi.