Thursday , 5th Jun , 2014

Tetemeko la Burudani ya nguvu ya muziki kupitia Kili Music Tour 2014, limeanza kuutikisa mji wa Kahama wakati huu ambapo imebaki siku moja tu kuelekea tukio la aina yake litakalofanyika Jumamosi hii ya tarehe 07, pale katika uwanja wa Halmashauri.

Kili Music Tour Kahama

Ziara hii gumzo ya muziki itawakutanisha wakazi wa Kahama na mastaa wakali watakaowasha moto jukwaani kama vile Shilole, Christian Bella, Madee, MwanaFA, AY, Rich Mavocal, Jambo Squad pamoja na Weusi.

Hii ni bonge moja la shoo, pale katika uwanja wa Halmashauri kuanzia saa 10 jioni, kwa kiingilio cha shilingi 2500 tu na kama hiyo haitoshi utapata zawadi ya bia yako moja ya Kilimanjaro Buree.

Kili Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu kwetu.