Monday , 2nd Jun , 2014

Baada ya wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya Kili Music Tour, katika uwanja wa CCM Kirumba makamuzi yanaelekea Kahama, Jumamosi hii ya Tarehe 07, katika uwanja wa Halmashauri.

Mwana FA akitumbuiza stejini

Kama ilivyo ada ya ziara hii ya muziki ya Kili itawakutanisha wakazi wa Kahama na mastaa wakali watakaowasha moto jukwaani kama vile Shilole, Christian Bella, Madee, MwanaFA, AY, Rich Mavocal, Jambo Squad pamoja na Weusi.

Itakuwa ni bonge moja la shoo, pale katika uwanja wa Halmashauri kuanzia saa 10 jioni, kwa kiingilio cha shilingi 2500 tu na kama hiyo haitoshi utapata zawadi ya bia moja ya Kilimanjaro Buree.

Kili Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu kwetu.