
Mwanamuziki huyo wa Pop mwenye umri wa miaka 31 amepata fedha hizo kutokana na ziara yake ya dunia ya Prismatic ambayo imeisha mwezi Oktoba, na malipo ya matangazo mbalimbali aliyoyafanya.
Akiongelea nafasi hiyo kama nyota aliyeendelea Katy Perry amesema anajivunia nafasi hiyo na kuendesha kampuni yake mwenyewe.
"Najivunia nafasi yangu kama bosi , kama mtu ninayeendesha kampuni yangu binafsi, mimi ni mjasiriamali na sioni aibu kwa hilo", alisema Katy Perry.
Msanii Beyonce ambaye mwaka jana alikuwa wa kwanza kwa kuingiza dola milioni 115, ameshika nafasi ya tano kwenye orodha hiyo kwa kuingiza dola milioni 54.5. Wasanii wengine waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo ni Lady Gaga, Jenifer Lopez na Miranda Lambert.