Saturday , 25th Apr , 2015

Rapa mkali kutoka nchini Kenya, Khaligraph amewataka mashabiki wake kutoka Afrika Mashariki kufahamu kuwa, hajalegeza kamba katika game ya Hip Hop, ujumbe ambao ameamua kuwafikishia kupitia mzigo wa freestyle ambao ameachia hivi karibuni.

Khaligraph Jones

Staa huyo mwenye michano tofauti, amesema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kufanya ngoma tofauti kwa muda na hivyo kupooza ushindani uliokuwa unaendelea katika muziki kwa upande huo na hapa anasema na mashabiki wake na vilevile mahasimu wake katika game.

Mbali na freestyle hii kwa mashabiki wake, Khaligraph katika mahojiano yake na East Africa Radio wiki hii amewataka mashabiki wake pia kufahamu ju ya mpango wake wa kufanya ngoma na msanii Proffesa Jay kutoka hapa Tanzania hivi karibuni.
Sehemu ya Freestyle ya kufungulia mwaka ya khaligraph