Tuesday , 24th Jun , 2014

Msanii wa muziki Juliani kutoka nchini Kenya, anatarajiwa kutoa mchango wa aina yake katika shughuli ya kueneza elimu ya umuhimu wa wanyamapori huko Kenya, katika kampeni za kupambana na ujangili ambalo pia ni tatizo la kitaifa Kenya.

Mwanamuziki wa nchini Kenya Juliani

Kampeni hizi zimepatiwa jina The Hands Off Our Elephants hususan kwa ajili ya kutetea maangamizi ya Tembo ambao wamekuwa wakiuawa kwa kasi na kutishia kutoweka kwa jamii hii ya wanyama.

Katika kampeni hii Juliani atashirikiana na wadau wengine kutoka sekta mbalimbali, akiwepo msanii wa uchoraji Chief Nyamweya ambaye naye atatumia usanii wake kufikisha elimu kwa jamii kuhusu tatizo la ujangili.