Wednesday , 12th Mar , 2014

Juliana Kanyomozi pamoja na mchekeshaji Anne Kansiime wa nchini Uganda wamepongezwa kwa jitihada zao za kufanya kazi kwa bidii na pia kutumia sanaa zao katika kusogeza mbele shughuli mbalimbali za maendeleo ya sanaa na nchi kwa ujumla.

Wasanii hawa wametakiwa kuendeleza moyo wao katika kazi zao na pia kuendelea kuwa mfano mzuri kwa jamii, hususan wanawake ambao kwa asilimia kubwa hujiweka nyuma kutokana na hofu na pia kutokujiamini kutokana na jinsia yao.

Pongezi hizi zinafuatia tukio la Anne pamoja na Juliana kupatiwa tuzo ya kutambuliwa mchango wa mwishoni mwa wiki kutoka kampuni maarufu huko Uganda, katika msimu huu wa mwezi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.