Wednesday , 1st Jul , 2015

Mtayarishaji video Joowzey ambaye kwa sasa anatamba kwa kazi mbalimbali ikiwepo Vise Versa ya Bonge la Nyau, ameibuka kujitetea juu ya tuhuma nzito juu yake kuhusiana na kuiga wazo la video 'High' ya msanii Eva Alordiah wa Nigeria.

mtayarishaji wa muziki wa nchini Tanzania Joowzey

Tuhuma hizo zinamweka mtayarishaji huyo njia panda haswa kuitumia video hiyo ya 'High' na kuigiza sehemu husika katika Video ya Tammy the Baddest "Down Low".

Baada ya mjadala na pia shutma ndefu mtandaoni kuhusiana na kitendo hicho, eNewz tumekutana naye na kumuuliza kulikoni? na haya ndio yakawa maelezo yake.