Witness a.k.a Kibonge Mwepesi,
Akizungumza na mwandishi wa EATV, Witness amesema kujiandikisha ni wajibu wao wasanii ili wapate kibali na kutambulika rasmi kwa kazi zao za sanaa, lakini pia waweze kushiriki EATV AWARDS, kwani itafikia hatua hata media hazitapokea kazi ambazo hazijasajiliwa.
"La kwanza wahakikishe wameenda kufanya registration BASATA, kwa sababu unajua mara nyingi watu tumekuwa tukibabia babia sanaa maana tulishaanza kucomplain kwa serikali jamani hii sanaa yetu, tulindieni kazi zetu na sisi tunafanya biashara, huwezi kuwa mfanya biashara bila kuwa na vibali na usajili, kwa hiyo hilo ni muhimu, kasajili jina lako ili mtu yeyote asitumie, ukapate kibali ili upate ruksa, na sasa hivi kunakoelekea hata ukitaka kutoa ngoma unatakiwa uwe na kibali, hata radio stations Tv stations hazitakwenda kupokea kazi ambazo hazijasajiliwa, na kwenye tuzo pia nimeona hicho kitu", alisema Witness.
Witness aliendelea kusema kuwa yeye alishasajili hivyo anawakumbusha wenzake kufuata agizo hilo la BASATA, zaidi atakwenda kulipia vibali vyake ili aweze kushiriki EATV AWARDS.
"Mi ntaenda kulipia tu vibali maana mimi mkongwe nimesajiliwa toka mwaka 2000 na ninajisifia kwa hilo, kwa hiyo wadogo zangu artist wote natoa wito, la pili pia angalieni ngoma zenu kali maana it is simple, maana mwaka jana mwezi wa 6 mpaka muda flani i know kuna ngoma kali, kwanza nitazileta kama mbili tatu natumai wataruhusu".