JCB amesema kuwa, mbali na wanamuziki wa kule kuwa na vipaji kamilifu katika kuimba na kupiga vyombo, pia mfumo wao unasimamiwa kwa namna ambavyo wanajionea matunda ya kazi zao.
JCB amekazia kuwa, mfumo kama huu umewapa thamani wasanii, kiasi kwamba ungelinganishwa na kazi ambazo wanazifanya wasanii hapa Bongo, marapa kama MwanaFA, Fid Q na wengine ambao amewatolea mfano akiwepo yeye, wangekuwa mamilionea.
JCB ameongeza kuwa, kwa sasa anajiendeleza kidongo huko Ulaya, Kimasomo na pia miradi yake, ikiwepo Brand ya 'Yani Kama Mbele Kabisa' ambayo amesema itakuwa ni kampuni kubwa ya nguo, mitindo pamoja na sanaa nyingine kipindi atakaporejea.