Saturday , 1st Mar , 2014

Dogo Janja aka Janjaro kama anavyopenda kujulikana kwa sasa, amesema kuwa baada ya kufikia umri ambao kwa sasa anaona kuwa ana uelewa na mambo wa kiutu uzima, ameamua kuendesha muziki wake kivyake nnje ya lebo ya mtanashati, huku akiwa na malengo kibao ya kuutumia muziki huu kujiendeleza kimaisha.

Kutoka katika maelezo haya, Dogo Janja pia amegusia swala la yeye kusitisha masomo yake kwa mara kadhaa sasa, ambapo amewataka watanzania kujua kuwa, katika historia yake hajawahi kusoma na kuvuka kidato cha tatu, huku akisisitiza kuwa anaelewa umuhimu wa shule na watu wasimsukume sana kwenda shule wakati wamemjulia kupitia muziki.

Dogo Janja amesema kwa sasa anahitaji kusimama mwenyewe ili kufahami anahitaji kupitia wapi na wapi ili kufikia katika mafanikio kimuziki.