Monday , 28th Dec , 2015

Nyota wa miondoko ya muziki wa Taarabu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, ametoa kichupa kipya kabisa cha kuuaga mwaka 2015 kilichobatizwa jina 'Nimpe Nani'.

Isha aka Jike la Simba anatambulisha kazi hii mpya kwa mara ya kwanza kupitia EATV ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wake wote kuukaribisha mwaka mpya ambapo pia amewashukuru sana wadau na mashabiki wote ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuusapoti muziki wake.

Mkali huyo amejipanga kufanya onyesho la muziki la kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka 2016 ndani ya wiki hii akiwasihi mashabiki wakae mkao wa kula.