
Idris Elba mwenye umri wa miaka 43 ambaye pia ni muongozaji wa filamu na rapa, atafanya ufunguzi wa tamasha hilo kwa kuchangamsha umati uliohudhuria kwenye viwanja vya Mercedes Benz huko Ujerumani, kwa ujuzi wake mkubwa wa DJ.
Sambamba na Idris Elba muigizaji Jessica Chastain nae anatarajiwa kuonekana kwenye tamasha hilo na kushiriki kwenye onesho la wimbo wa Unapologetic Bitch.
Amy Schumer na mwimbaji ambaye wiki hii ametangazwa kuwa mwanamuziki wa kike ambaye ameingiza pesa nyingi kwa mwaka huu wa 2015 Katy Perry, ameungana na Madona kwenye tamasha hilo ambalo lilizinduliwa rasmi wiki iliyopita nchini Uingereza na linatarajiwa kufanyika nchi 11, na linatarajiwa kukamilika mwaka 2016.