Thursday , 30th Apr , 2015

Msanii mkongwe na mtaalam wa kucharaza tarumbeta Afrika Hugh Masekela, kutoka Afrika Kusini, anatarajiwa kutua nchini Uganda siku ya Jumatatu, tayari kwa ajili ya kufanya onesho kubwa kabisa nchini humo.

Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz nchini Afrika Kusini Hugh Masekela

Msanii huyo katika wakati wake huko Uganda, ataonesha uwezo wake mkubwa kwa onesho katika tamasha la Jazz It UP, akishirikiana na msanii Isaiah Katumwa atakayekuwa akiadhimisha miaka 20 toka kuanza kufanya kazi ya muziki.

Kwa upande mwingine pia Hugh mwenye umri wa miaka 75 sasa, kutokana na uzoefu na ujuzi mwingi katika kazi yake hiyo muziki, hivi karibuni pia ametunukiwa udaktari wa nne wa heshima katika fani ya muziki kutoka chuo kikuu cha Rhodes.