Tuesday , 2nd Sep , 2014

Tamasha kubwa kabisa la burudani ya muziki wa nyumbani, Kili Music Tour 2014 baada ya kuzunguka mikoa 9 sasa linahitimishwa na show ya fainali, itakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club Jumamosi hii.

Kili Music Tour 2014 Tanzania

Jukwaa litashambuliwa vilivyo na Ommy Dimpoz, Prof Jay, Ben Pol, Mwana FA, AY, Rich Mavoko, Malkia Khadija Kopa, Jambo Squad,Vanessa Mdee, Christian Bella, Mashujaa Band, na Weusi.

eNewz imetimba mitaani kupima joto la amsha amsha ya Kili Music Tour 2014, kwa wapenzi wa Burudani katika jiji la Dar es Salaam ambapo watu wamekabidhiwa zawadi za Tiketi, T-shirt ya Kilimanjaro, T-shirt ya East Africa Radio pamoja na fedha taslim.

Kumbuka kuwa tamasha zima la Kili Music Tour litaanza kutimua vumbi Jumamosi hii majira ya saa 10 jioni kwa kiingilio cha buku tatu tu Mlangoni, na utapata bia moja ya Kilimanjaro Mlangoni Buree, na kisha bonge moja la burudani, Tunazungusha Kikwetu kwetu pale Leaders Club, hii sio ya kusimuliwa Jipange.