Saturday , 7th Jun , 2014

Staa wa Movie na msanii wa Muziki hapa Bongo, Hemedy PHD, ametangaza zawadi kwa wapenzi wa kazi zake hususan katika muziki kuanzia mwezi huu mpaka mwaka utakapoisha.

Hemedy PdD

Hemedy amesema kuwa, ametayarisha mzigo wa video sita za muziki ambazo zitakuwa zinatoka moja moja kila mwezi mpaka mwaka utakapoisha.

Kuhusiana na mchongo huu, Huyu hapa Hemedy mwenyewe amesema kuwa kwa sasa nanafanya video yake ya tatu ambayo inakwenda kwa jina Highup zikiwa zimebaki nyingine tatu kwaajili ya mpango huu wenye lengo la kuwaonesha mashabiki wake kuwa kwa sasa ameamua kuwa serious zaidi na muziki.

Hemedy pia amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wa video yake ya On My Wedding Day inayotoka leo, habari kubwa nyingine ikiwa ni kuwa project hizi zote za video zitafanywa na Kwetu Studioz.