Monday , 24th Feb , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Harriet Kisakye amethibitisha dhamira yake ya kuingia katika siasa, ambapo ameweka wazi kuwa mwaka 2016, atagombea kiti cha ubunge wa jimbo la Wakiso huko Uganda.

Harriet ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kupitia kazi yake inayokwenda kwa jina Kinigeria, amesema kuwa atasimama kama mgombea huru na ana uhakika kuwa ana nafasi ya kumshinda mtu yeyote atakayepambana naye kuchukua nafasi hii.

Kisakye ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 34 tayari ameanza kwa nguvu mikakati ya kujipatia nafasi hii muhimu katika siasa, huku akitegemea ushawishi alionao kupitia muziki alionao, kumsaidia kupata wafuasi.