Tuesday , 25th Mar , 2014

Nyota wa muziki wa nchini Kenya, Habida baada ya kutangaza kupiga dili kubwa ya uigizaji ndani
ya moja ya tamthilia kubwa kabisa Afrika, ameweka wazi kuwa, fani hii ya uigizaji ni kitu
ambacho amesomea.

Habida

Habida amesema kuwa, kisomo chake katika uigizaji kimefika ngazi ya shahada kutoka chuo mahiri huko Marekani ambapo pia amekwishafanya kazi na msanii na mtayarishaji filamu mahiri, Tyler Perry.

Habida amesema kuwa, Fani hii ya uigizaji ameisomea huko Marekani, na amekuwa na wakati mgumu kushiriki katika maigizo, tamthilia ama filamu mbalimbali hapa Afrika kutokana na malipo madogo ambayo waigizaji hupewa.

Habida amesema kuwa, ana uzoefu na elimu kubwa si kutoka Marekani tu, bali pia London ambapo
huko pia alijipatia cheti kutoka kozi nyingine maalum ya masuala ya uigizaji.