Sunday , 6th Jan , 2019

Baada ya siku 1 kupita tangu msanii wa Hip Hop Bongo AY' aweke wazi alivyoanza harakati zake za muziki jijini Dar es salaam kwa kuishi kwenye Kontena, msanii mwenzake Fareed Kubanda maarufu Fid Q amemshauri alinunue Kontena hilo.

AY akiwa kwenye Kontena ambalo aliishi mwaka 1999

Fid Q ambaye bado yupo kwenye fungate la 'Honey Moon' baada ya kufunga ndoa wiki hii, amemshauri mkongwe mwenzake huyo alinunue Kontena hilo kisha atengeneze Studio kwaajili ya wasanii wanaotoka mikoani.

''Nimemshauri AY alinunue lile Kontena kisha aligeuze studio na kijiwe maalum kwa ajili ya wasanii wote wanaotoka mikoani na kuja dar Kwa ajili ya kuendeleza harakati zao za sanaa'', ameeleza Fid Q.

Jana kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii AY aliweka wazi kuwa alikuja Dar es salaam mwaka 1999 kwaajili ya kuendeleza kipaji chake lakini hakuwa na pakufikia ikabidi awe analala kwenye Kontena moja maeneo ya Upanga.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Heri ya Mwaka Mpya Ndugu zangu. Leo ngoja niwaambieni story kwa ufupi jinsi Ambwene baadaye akawa AY alivyokuja kupambana na maisha Jijini Dar Es Salaam. Nilikuja Dar mwaka 1999 kutoka nyumbani Morogoro kwa msukumo wa Ndugu yangu @gzingalize ambaye tulikuwa tunasoma wote Ifunda Technical School IRINGA. Nilikuja Dar nikiwa na ndoto moja tu ya kufanikiwa kupitia kipaji changu cha Muziki. Nilipofika sehemu niliyoanza kuishi ni kwenye Container hili hapo nyuma lipo Upanga baada ya mataa ya California Dreamer kama unaenda mjini na ndio sehemu nilikaa kwa kipindi kirefu kabla sijapewa hifadhi kwa familia ya @gzingalize halafu nikahamia kwa kina @kingcrazy_gk. Container hili lilikuwa linatumiwa na mafundi wa kushona nguo. Hivyo kila siku ilikuwa ni lazima niamke saa kumi na mbili asubuhi kabla Mafundi hawajafika. Pia ilibidi kuoga ilikuwa kutembea mpaka MNAZI MMOJA kwenye mabafu ya Jumuiya yaliyoko pale ya kulipia. Mwisho wa siku ilikuwa lazima ndoto itimie bila kujali mazingira husika. NI MUHIMU KUSHUKURU KWA KILA JAMBO MUNGU ANALOKUBARIKI NALO NA KUWEKA BIDII KWENYE NDOTO ZAKO PERIOD!!..  @shaffieweru #Safari 

A post shared by A.Y (@aytanzania) on