Zahir Ally Zorro
Zorro ameyasema hayo alipokuwa akizungumzza na EATV kuhusu mtazamo wake juu ya kuanzishwa kwa tuzo hizo.
“EATV AWARDS ni kitu muhimu sana kwa taifa zitasaidia sana wasanii kutambulika ndani na nje ya nchi kutokana na uzito wa tuzo pamoja na washiriki watakaowania tuzo hizo” Amesema Zoro
Aidha Zorro ameongeza kuwa pia wasanii watakaofanikiwa kuingia katika tuzo hizo watapata faida kubwa kwani hata watu watakao taka kuwapa show lazima watazingatia pia thamani ya tuzo ambazo walishawahi kupata.
