Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema anajivunia kitendo cha baba yake kumuachia urithi wa 'nguvu', kwani ameweza kuwa na watoto wengi.
"Kitu ambacho mzee ameniachia na najivunia ni kuwa na nguvu za kuwa na watoto wenGi, tayari nina watoto wengi na bado wengine watakuja”, amesema Dully Sykes.
Baba Mzazi wa Dully Sykes ,ambaye pia alikuwa msanii na kipenzi cha watu, Mzee Abby Sykes alifariki dunia Februari 15, 2015, baada ya kuugua muda mrefu.