Saturday , 8th Nov , 2014

Baada ya kimya cha muda sasa toka Rapa Dogo Janja arejee ndani ya chama kubwa la Tip Top Connetion, Madee ameweka wazi kuwa, katika siku za usoni kabla mwaka haujaisha, kutakuwa na kazi mpya kutoka kwa rapa huyu kinda, ikifuatiwa na project yake.

Madee na Dogo Janja

Madee amesema haya katika mahojiano tuliyofanya naye, akiwaahidi wapenzi wa burudani ya muziki kuwa, kwa sasa wameweka kipaumbele katika kumaliza kazi ya Dogo Janja, ambayo itafuatwa na rekodi yake, kazi ambazo zitakuwa gumzo katika kufungia mwaka 2014.