Friday , 8th Jul , 2016

Dj maarufu na mkongwe hapa nchini Tanzania John Dilinga a.k.a Dj JD amewataka Ma DJ nchini kuheshimu kazi zao na kuepuka anasa zisizo na maana zinazoweza kuwaharibia kazi.

DJ John Dilinga

DJ JD ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalumu na Planet Bongo ya EA Radio akitumia fursa hiyo pia kumtakia DJ wa EATV na Radio Ommy Craizy mafanikio mema kwa kukumbuka siku ya kuzaliwa kwake.

Kati ya watu ambao niliona wanaweza kufika mbali ni DJ Ommy Crazy na mara nyingi nilikuwa nikikutana naye huwa ananiambia brother nataka unisaidie yale maujanja yako hivyo ninapomuona sasa ana shine si shangai.

Aidha DJ JD amewashauri Ma DJ nchini wawe ni watu wanaopenda kujifunza vitu vipya mara kwa mara na pia waepuke anasa za ulevi na umalaya kwa kuwa kuna watu wanachukulia kazi hizi ni kazi za anasa hivyo nizamu ni kitu muhimu sana katika kazi hii.