Saturday , 22nd Nov , 2014

Msanii wa muziki Diamond Platnumz ameongea na eNewz kuhusiana na hali ya mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa, na kusema kuwa swala hili ni la watu wawili na ataweka wazi baadhi ya mambo nyeti katika mahusiano hayo wakati rasmi ukifika.

Diamond Platnumz na Wema Sepetu

Kauli hii inakuja kufuatia kipindi hiki ambapo kuna tetesi na hisia tofauti juu ya kuwepo kwa maelewano hafifu kati ya staa huyu na mpenzi wake anayejulikana rasmi, Madame Wema Sepetu

Kwa kuendelea kufahamu juu ya hili kwa undani zaidi, fuatilia kipindi cha uhalisia cha Madame Wema Sepetu, In My Shoes kinachoruka kupitia hapa hapa EATV, kila Ijumaa saa 3 na nusu usiku.