Saturday , 7th Jun , 2014

Kufuatia kuibuka kwa mkanganyiko kuhusiana na baba halisi wa mtoto wa mwanamuziki Desire Luzinda wa nchini Uganda, staa huyu ameamua kuibuka na kuweka mambo sawa, ambapo amemtaja Michael Kaddu kuwa ndiye baba halali wa mtoto wake.

Dezire

Desire amesema kuwa, anamtambua Michael na hafamu chochote kuhusiana na mwanaume anayefahamika kwa jina Juma Seiko ambaye hivi karibuni aliibuka na kujitambulisha pia kama baba wa mtoto wa mwanamuziki huyu na kuzua mkanganyiko mkubwa.

Katika maelezo yake, Desire ambaye anajikwamua kusafisha jina lake, amemshangaa Juma Seiko, na kuhoji ni wapi mwanaume huyu alikuwepo wakati wote mpaka sasa alipoamua kuibuka kujitangaza kama baba wa mtoto wake.