Tuesday , 10th Jun , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Desire Luzinda baada ya kupata mafanikio makubwa katika onesho lake mwisho wa wiki, ameibuka na kutoa ya moyoni kwa wale wote waliokuwa wanaeneza maneno kuwa onesho hili litafeli.

Desire Luzinda akiwa katika pozi

Desire kwa njia ya mtandao amewashukuru mashabiki wake na wasanii ambao wamesapoti onesho hili ambalo kwa sasa limekuwa gumzo katika kona za Mitaa ya Jiji la Kampala.

Desire alilazimika kukabiliana na changamoto za onyesho lake kutabiriwa kufanya vibaya, hasa kutokana na onesho hilo kufanyika siku chache baada ya onesho lingine la Msanii Judith Babirye kupata muitikio mdogo sana wa watu katika eneo hilo hilo.