Friday , 28th Nov , 2014

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Nirvana EATV, aliyebobea katika masuala ya Fashion, Deogratius Kithama, ameingia katika kinyanyanyiro cha tuzo za Swahili Fashion Week, katika kipengele cha mwandishi bora wa mwaka wa habari za mitindo.

mtangazaji wa kipindi cha Nirvana cha EATV Deogratius Kithama

Zoezi la upigaji kura kwa wanaowania tuzo hizi tayari limekwishaanza ambapo unaweza kumpigia kura Deogratius kumuwezesha kushinda tuzo hii kwa kutuma kwa njia ya ujumbe mfupi namba yake ya ushiriki SFWFJ03 kwenda namba 15678.

Tuzo hizi pia katika vipengele mbalimbali zinahusisha mastaa wakali kabisa kama vila Diamond Platnumz, Wema Sepetu na JUma Jux ambapo pia unaweza kuona orodha nzima ya washiriki na kuwapigia kura kupitia tovuti wa Swahili Fashion Week.