Monday , 8th Jun , 2015

Star wa muziki Davido kutoka nchini Nigeria, amekuwa mfano wa kuigwa na wengi hasa baada ya kufanikiwa kuhitimu shahada ya daraja la kwanza kutoka idara ya muziki ya Chuo Kikuu binafsi cha Babcock huko Nigeria.

msanii wa muziki wa nchini Nigeria Davido akitabasamu kwa kuhitimu shahada yake

Star huyo amepata pongezi nyingi kwa hatua hiyo kutoka kwa mastaa wenzake, akiwepo Runtown, Tiwa Savage kati ya wengine, huku mchekeshaji Bascketmouth akitania kuhusiana na tukio hilo kwa kusema hatua aliyopiga Davido imemfanya kurudia vitabu akiwa na imani ya kuwa mtaalam wa fani mbalimbali kwa wakati mmoja.

Meneja wa staa huyo, Kamal Ajiboye na mtayarishaji muziki Shizzi kutoka timu ya Davido ya HKN nao pia wanatarajia kuhitimu masomo yao kutoka kitengo cha muziki cha chuo hicho mapema mwaka kesho.