Tuesday , 6th Dec , 2016

Shangwe za usiku wa EATV AWARDS zinazidi kutawala mjini ambapo leo wanasanii watakaowasha moto jukwaa hilo kwa kutoa burudani kali wametajwa.

Darassa

Burudani hizo zitapambwa na msanii ambaye hivi sasa ndiye 'talk of the town', ambaye pia wimbo wake nusura utoe roho za watu kwa ajali baada ya dereva kuacha usukani na kucheza wimbo wa 'MUZIKI' wa Darassa au 255 Champion.

Darassa atatoa burudani za kufa mtu za kufungia mwaka, sambamba na mzee wa kuzima simu feki na kupiga CHAFU POZI, Bill Nas.

Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki kwa pamoja itashuhudia wasanii hao wakitoa burudani, pamoja na wasanii wengine ambao watatangazwa siku zijazo, huku watu mbalimbali maarufu wakihudhuria sherehe hizo, ambao wengine itakuwa ni 'suprise'.

Bill Nas

Tags: