Wednesday , 7th Oct , 2015

Nyota wa muziki wa Rap, Darasa ametoa tathmini yake kuhusiana na suala la wasanii kutumika katika majukwaa ya kisiasa kwa sasa, akiwataka kuwa waangalifu kwa kutokujikita kutazama faida ya sasa ambayo itapoteza maslahi yao katika siku za baadaye.

Nyota wa muziki wa Rap nchini Darasa

Darasa ametoa somo hilo kwa wasanii wenzake kutumia pia akili zao pale wanapotumika na kupima hali ya mambo endapo katika pande walizochagua, maslahi yao yatakuwa endelevu ama watakuwa wanapoteza nguvu sasa na kujutia hapo baadaye.

Darasa amezungumza kwa kirefu zaidi juu ya hili na kipindi cha Planet Bongo, na eNewz inakuonjesha kwa ufupi tu tathmini ya nyota huyo.