Wednesday , 13th Aug , 2014

Msanii wa muziki Damian Soul amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, muziki wake wa sasa umebadilika kwa kiasi kikubwa, mfano ukiwa ni ngoma yake ya Dua la Kuku, ambayo ni mchanganyiko wa ladha mbalimbali kutoka barani Afrika.

msanii wa muziki nchini Tanzania Damian Soul

Damian ambaye ni mkali wa miondoko ya Soul anayeamini kuwa muziki ni hisia, amefafanua kuwa, aina hii ya muziki ambayo amefanya sasa ni Afrosoul ambayo ni hatua kubwa ya mabadiliko kutoka kwa Damian Soul ambaye mashabiki tayari wamekwishamzoea.