Thursday , 30th Apr , 2015

Cyrill Kamikaze, ametoa kauli inayotetea wasanii wanaoendesha sanaa zao kwa skendo, na kusema kuwa tabia hiyo ni kutokana na watanzania wengi kuvutiwa zaidi na tetesi, ama uvumi kuhusu maisha binafsi ya wasanii.

Msanii wa bongofleva nchini Cyril akiwa na rafiki yake

Staa huyo ambaye binafsi amesema haamini katika 'skandali' ili kutoka, ikiwa pia hivi karibuni ametoka katika skendo ya kujingiza katika mahusiano na staa wa filamu Sabby Angel, amesema kuwa wasanii hufanya hivyo ili waongelewe, yeye binafsi akiwa haamini suala hilo.

Cyril kwa sasa amerejea kwa kishindo na video yake mpya inayokwenda kwa jina Nikikuona aliyoifanya nchini Kenya chini ya director Young Wallace.